Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

SIKU 26 YA 31

Maisha ya watakatifu, watu waliokubali kumfuata Yesu Kristo yanajaa faraja na kutiana moyo. Tena yanajaa ushuhuda. Ushuhuda mwema huanzia pale tulipo. Kusameheana kunakojenga na kufariji kunaasilika katika msamaha unaopatikana kwa Yesu Kristo. Hakuna dhambi ambayo haisameheki kama ikitubiwa kwa nia ya kweli. Msamaha huu unaenea nje ya kanisa. Kutoa na kupokea msamaha iwe ni tendo la daima. Linganisha soma la leo kuanzia m.5 na Mt 6:12 ambapo Yesu anatufundisha kuomba ombi hili, Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz