Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

SIKU 31 YA 31

Wahubiri, waalimu na wote wanaoshuhudia juu ya Yesu Kristo wanapaswa kukumbuka kwamba wanasimama mbele na katikati ya uwepo wa Mungu. Hivyo, wakati wote tunaposhuhudia juu ya Yesu Kristo tunapaswa kuwa waangalifu. Kuharibu, kupotosha na kupindisha Neno la Mungu huja ili kujipendekeza au kuridhisha wasikilizaji. Tumeitwa kutangaza kweli ya Neno la Mungu na si vinginevyo. Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli(Yn 8:31-36).

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana