Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

SIKU 14 YA 31

Ni muhimu kuwa waangalifu na manabii, pia siku hizi. Wale wasiotumwa na Mungu wana alama zao: 1.Hunena ya mioyo yao (m.2). 2.Hufuata roho yao wenyewe (m.3). 3.Hufikiria maslahi yao badala ya kujenga kilichobomoka na kutibu magonjwa ya kiroho (m.5-6:Hamkupanda kwenda mahali palipobomolewa, wala hamkuitengenezea nyumba ya Israeli boma, wapate kusimama vitani katika siku ya Bwana.Wameona ubatili, na uganga wa uongo). 4.Huona uongo (m.7:Je! Hamkuona maono ya bure, hamkunena mabashiri ya uongo? Nanyi mwasema, Bwana asema; ila mimi sikusema neno). 5.Huwapotosha watu kwa kuwahubiria amani na kusifu kazi yao bovu (m.10: Wakisema, Amani; wala hapana amani; na mtu mmoja ajengapo ukuta, tazama, waupaka chokaa isiyokorogwa vema). Tumwombe Mungu atuongoze tuweze kupambanua ni nani ametumwa kweli. Kama tukiwakubali tu manabii wa uongo, hatutaepuka ghadhabu ya Mungu juu yao.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz