Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano
Nabii ni mfano hata kwa jinsi anavyokula na kunywa kwa woga. Lakini watu wanapoifanya mioyo yao kuwa migumu wanashindwa kupokea ujumbe wa Mungu unaoletwa kwao. Waisraeli walidhania huo ni wa muda mrefu sana ujao au hata kwamba maono yote hayatimizwi(m.22). Lakini sisi tunaojua historia ya Israeli twajua pia kuwa Mungu hachelewi wala hawahi. Anayosema yatakuwa. Hakika tutaona utimilizo wa maono yote(m.23). Tusipuuze kuwa Mungu anategemea watu wajidhili, waache uasi na kufikilia toba.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz