Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

SIKU 12 YA 31

Ezekieli na baadhi ya Waisraeli walikuwa uhamishoni kule Babeli. Hapo nabii alikuwa ishara ya onyo kwa Waisraeli waliokaa Yerusalemu bado. Hata hawa watachukuliwa mateka na kwenda uhamishoni kama Ezekieli anavyohamishwa kimfano na Mungu. Sababu ni uasi wao. Mfalme Sedekia ametajwa kipekee (2 Fal 24:18-20:Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Hamutali, binti Yeremia wa Libna.Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Yehoyakimu.Maana kwa sababu ya hasira ya Bwana mambo hayo yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata alipokuwa amewaondosha wasiwe mbele ya uso wake; naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli). Hayo yatakapotokea, waasi watajua kwamba Mungu ndiye Bwana. Pia atajisazia watu watakaokuwa ushuhuda. Tujitathmini ni kwa jinsi gani tunakuwa washuhuda wa kazi za Mungu mahali tulipo.

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz