Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

SIKU 30 YA 30

Ayubu anao ujasiri ambao ni kwa nadra kuushuhudia miongoni mwa wanadamu, hata kwao wanaodai wenyewe kuwa wako karibu na Mungu. Anaikubali na kuiopokea hali inayomkabili. Anakiri ukuu na mamlaka ya Mungu dhidi yake. Hata hivyo Ayubu ana hakika kuwa Mungu angemsikiliza, Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake? La, lakini angenisikiliza(m.6). Shida ni moja tu kwamba Mungu amejificha, na Ayubu hamwoni. Tazama, naenda mbele, wala hayuko; narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; hujificha upande wa kuume, hata nisimwone(m.8-9; ling. Zab 10:1, Ee Bwana, kwa nini wasimama mbali? Kwani kujificha nyakati za shida?). Msingi wa imani ya aina hii ni kuamini kuwa yanayotokea yana lengo la kusafisha, kuimarisha na kujenga kwa upya imani ya mwaminifu.

siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz