Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano
Daudi yuko katika hali ya kuomboleza sana. Maisha yake yako hatarini kabisa. Na kilio chake anakitoa kwa Mungu. Anamfunulia moyo wake. Yuko imara katika imani. Ina maana ya kwamba akiwa na mafanikio humshukuru na kumwimbia Mungu. Na akiwa taabuni vilevile humwelekea Mungu akimtolea maombi yake na kilio chake. Haendi kwa miungu wala kwa waganga. Mungu ndiye tegemeo lake katika hali yoyote ile (Yak 5:13-15, Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa). Kwa kumtegemea Mungu hivi, Daudi amejifunza kwamba yu mwaminifu, mwema na mwenye uwezo wa ajabu (m.13, Maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, wakati ukupendezao; Ee Mungu, kwa wingi wa fadhili zako unijibu, katika kweli ya wokovu wako)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz