Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano
Maadui wanaowazunguka waaminio hawana jipya. Elifazi anamsuta Ayubu kwa kuonesha kuwa Mungu hamhukumu mcha Mungu, Je! Ni kwa wewe kumcha yeye anakukemea? Na kuingia hukumuni nawe?(m.4). Sasa ni wazi kwamba Ayubu anateswa, basi, siye mwenye haki! Ndiyo maana ya swali la Elifazi. Basi, kuanzia m.5 anataja dhambi ambazo huenda Ayubu amewahi kuzitenda. Lakini mashtaka haya hayamsaidii Ayubu, bali Elifazi anaidhoofisha na kuinyong’onyeza tu imani ya Ayubu. Lakini Ayubu hayumbishwi. Msimamo wake ni huu: Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu; sina wema ila utokao kwako (Zab 16:2).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz