Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano
Mara nyingi Agano Jipya hutaja mistari kutoka Agano la Kale ili kuonyesha jinsi maneno ya manabii yalivyotimizwa. Pia Yesu Kristo alifanya hivi (mfano ni Luka 24:25-27 anaposema Yesu, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe). Maneno kutoka Zaburi yametajwa sana katika Agano Jipya (mfano ni Lk 24:44-47 anaposema Yesu, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu). Zaburi ile iliyotumika mara nyingi zaidi katika Agano Jipya, ni Zaburi 22. Na baada ya Zaburi hii inafuata Zaburi ya 69! Jaribu kwa mfano kulinganisha m.9 unaosomeka, Wivu wa nyumba yako umenila, na laumu zao wanaokulaumu zimenipata, na maneno yafuatayo: Wanafunzi wake [Yesu] wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila(Yn 2:17). Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi(Rum 15:3). Au chukua m.21 unaosomeka, Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki, na linganisha maneno hayo na Yohana 19:28-29, Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani. Ni kweli kama Yesu alivyosema siku nyingine, Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe (Lk 21:33).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz