Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

SIKU 28 YA 30

Mashtaka dhidi ya Ayubu yanaendelea. Ukiwa na imani isiyo thabiti, unaweza ukafikia hatua ya kuamini kuwa Mungu yuko mbali, hajali, haangalii, hahusiki nawe. Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu?Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu(m.13-14). Kumbe, hakuna cha kuficha kwake. Hakuna kisicho wazi mbele yake. Uumbaji uko chini yake. Waliokata tamaa hudhani Mungu hufungwa na mipaka, wakati na historia. Mungu hujibuje? Zingatia Zab 139:12, Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku nao huangaza kama mchana, Giza na mwanga kwako ni sawasawa. Tafakari pia maana ya Isa 66:1-2,Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz