Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

SIKU 26 YA 30

Zaburi ya 120 hadi 134 ziliimbwa na waabudu walipokuwa safarini kwenda Yerusalemu wakati wa sikukuu. Zaburi hii inaadhimisha ulinzi wa Mungu katika maisha mazima. Msafiri anapitia nchi yenye milima akikumbuka kwamba Mungu aliyeumba milima yote atamhifadhi na kumsaidia daima. Hata usiku akilala kando ya njia Mungu ambaye kamwe halali usingizi, hukesha juu yake. Mungu atamlinda katika hatari zote usiku na mchana. Katika safari yake atamleta Yerusalemu salama na hata kumrudisha nyumbani kwake tena.

Andiko

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz