Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

SIKU 29 YA 30

Mdhihaki wa Ayubu anaona kuwa majaribu yaliyompata yanaasilishwa na kukosa imani. Aonavyo, amani, wema na mafunzo yamekosekana. Maoni yake ni ya kweli kiasi hiki kwamba mtu ni mdhambi, naye anahitaji toba (m.23,Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa). Hakika Mungu anawainua waangukao na kuwaokoa wanaonyenyekea.Hapo watakapokuangusha, utasema, Kuna kuinuka tena; naye mnyenyekevu Mungu atamwokoa(m.29). Ayubu ameshaonesha hayo kwa Mungu (Ayu 7:20). Lakini Elifazi hana maarifa sahihi kuhusu hali hii. Katika m.30 anasema, Utaokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako. Lakini usafi wa mikono haumwokoi mtu, wala hana uhakika wa kufanikiwa kama Elifazi anavyodai katika m.28, Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; na mwanga utaziangazia njia zako.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz