Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

SIKU 23 YA 30

Mungu ni mhukumu wa haki. Tajiri kwa maskini, kila mmoja hupokea kwa kadri ya mwenendo wake mbele za Mungu. Lakini mara nyingi haki hiyo imefichwa tusiione sisi. Fikiria tofauti anayoonesha Ayubu katika m.23-25: Mmoja hufa katika nguvu zake kamili, mwenye kukaa salama na kustarehe;vyombo vyake vimejaa maziwa, na mafuta ya mifupani mwake ni laini.Mwingine hufa katika uchungu wa roho, asionje mema kamwe. Haki ikoje? Tuzingatie kuwa Mungu ndiye ajuaye atakavyoupatiliza uovu. Huwavumilia waovu, akiwapa nafasi ili watubu (2 Pet 3:9, Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba). Kifo cha kimwili hakioneshi kila kitu. Adhabu ya dhambi ni mauti ya milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu(Rum 6:23). Uzima wa milele ni karama ya Mungu ambayo hakuna aistahiliye.

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz