Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano
Sofari alisema mafanikio ya waovu ni ya muda mfupi tu. Ayubu anampinga, maana anaona watu hao hufanikiwa katika hali zao zote, hata wakimwambia Mungu kwamba hawamhitaji. Jambo muhimu la kujifunza hapo ni kwamba mafanikio ya kidunia hayapaswi kuhusishwa na wema wa mtu mbele za Mungu. Viwango anavyotumia Mungu kuhesabu mafanikio, havijengwi juu ya ustawi wa kimwili bali wa kiroho. Mtu anayepata kibali kwa Mungu ndiye mwenye utajiri wa kweli. Huo wadumu milele, bali ule wa dunia huishia duniani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz