Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano
Sofari hakatai kuwa waovu wanaweza kutajirika, lakini furaha yao ni ya muda mfupi tu. Hata maneno haya ya Sofari hayamsaidii Ayubu ambaye hakuwa mkosaji kama alivyoshutumiwa. Lakini ni kweli, njia ya mwovu ijapoonekana ya mafanikio, ina mwisho mchungu. Hata kama akionekana kustawi hadi kifo chake, tukumbuke kuwa mwanadamu ana maisha ya duniani na ya nchi nyingine baada ya dunia. Hukumu ya kuteswa na kutengwa na Mungu milele ndiyo fungu la waovu baada ya dunia (m.7a, Ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe). Nini hatima yako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz