Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano
Kuna faraja kubwa kwa mtu anayeteseka akiwa anamwamini Yesu na kuenenda katika haki. M.25-27 inaonyesha tumaini la kweli kwa mtu huyo: Mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;nami nitamwona mimi nafsi yangu, na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu.Ayubu anajua mteteaji wake yu hai. Ndiye Kristo Yesu. Inaonekana Ayubu anategemea kumwona baada ya yeye kufa kimwili. Kumbe, mateso yetu ya kitambo kidogo hayapaswi kuyaondoa macho yetu katika mede ya utukufu iliyoko mbele yetu. Punde kidogo, magumu ya mwilini yatapita, na kufumba na kufumbua, tutaingia katika burudiko tutakapokuwa tunafarijiwa na Yesu Kristo milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz