Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano
Roho wa Mungu hushuhudia pamoja na roho za wanaomwamini Yesu kwamba ni wana wa Mungu (Rum 8:16; Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu). Je, maana yake ni kwamba hata kama watateseka katika mwili, na watu watawaongezea maumivu kwa maneno ya kuvunja moyo, wahanga wa majaribu hubaki na faraja kubwa mioyoni mwao wakitambua uhusiano wao na Mungu ni imara? Hakika Ayubu hakujitambua hivyo. Hata anasema ni Mungu aliyemtendea vibaya zaidi (m.6, Jueni basi kuwa Mungu amenipotosha, na kunizingira kwa wavu wake). Lakini hata katika hali hii, Ayubu anaendelea kumkimbilia Mungu na kumlilia. Tufuate mfano wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz