Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
Lakini mimi niliona kwamba hakutenda neno la kustahili kuuawa (m.25). Hali ya mtume Paulo inafanana na hali ya Yesu. Maana mashtaka ya Wayahudi hayakuwa na msingi na hayakuweza kuthibitishwa: Wale Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemu ... wakaleta mashitaka mengi mazito juu yake [Paulo], wasiyoweza kuyayakinisha(m.7; ling. na Yn 19:6 ambapo Yesu anatendewa vivyo hivyo: Wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake). Walionekana kama watu wanaomwabudu Mungu sana, lakini ukweli ni kwamba walitawaliwa na nguvu ya Shetani (unaweza kusoma zaidi katika Yn 8:37-47). Kwa sababu hii walimpinga sana Roho Mtakatifu na ile nuru ambayo walikutana nayo katika Yesu Kristo na mtumishi wake Paulo. Je, Yesu kweli ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz