Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
Mtume Paulo alikuwa na busara kama nyoka kama Yesu alivyoagiza: Iweni na busara kama nyoka(Mt 10:16). Busara hii ilionekana kwa jinsi alivyosisitiza sana juu ya ufufuo wa wafu: Ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo, Ee Mfalme. Kwa nini limedhaniwa kwenu kuwa ni neno lisilosadikika, kwamba Mungu awafufua wafu?(m.7-8). 1. Katika kulisisitiza hili alikuwa mkweli maana ufufuo wa Yesu ni jambo la msingi kabisa katika Ukristo (1 Kor 15:16-20). 2. Jambo hili limetabiriwa na manabii wa Agano la Kale. Kwa hiyo Paulo hakupingana na maandiko matakatifu ya Wayahudi (utabiri kuhusu ufufuo unapatikana katika k.mf. Zab 16:9-11 na Dan 12:1-4). 3. Wayahudi walishindana juu ya suala hili la ufufuo. Hivyo Paulo alivunja umoja wao: Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu. Alipokwisha kunena hayo palikuwa na mashindano baina ya Mafarisayo na Masadukayo, mkutano ukafarakana. Kwa maana Masadukayo husema ya kwamba hakuna kiyama wala malaika wala roho; bali Mafarisayo hukiri yote. Pakawa na makelele mengi. Waandishi wengine wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakateta, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema naye, ni nini?(23:6-9).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz