Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 7Mfano

Soma Biblia Kila Siku 7

SIKU 30 YA 31

Walikuwa wanasafiri kwa merikebu yaani meli. Kwa hali ya wakati ule ilikuwa meli kubwa. Walikuwemo watu 276 (m.37). Meli za wakati ule hazikuwa na injini. Zilitegemea nguvu za upepo tu. Upepo ulitekwa na matanga. Kwa vile walitegemea sana hali ya hewa safari ziliweza kuchukua muda mrefu. Safari ya Paulo na wenzake haikwenda upesi. Walipokuwa wanafika kisiwa cha Krete wakati wa baridi ulikuwa umekaribia ambao una upepo mkali na tufani. Hawakusikiliza maonyo ya Paulo (m.9-11:Paulo akawaonya, akawaambia, Wanaume, naona kwamba safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia. Lakini yule akida akawasikiliza nahodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyoyasema Paulo.). Wakaingia katika hali ngumu sana (m.20: Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka).

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 7

Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz