Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
Paulo hakujisifu kwa ajili ya kazi yake bali alimpa Mungu utukufu: Kwa kuwa nimeupata msaada utokao kwa Mungu nimesimama hata leo hivi nikiwashuhudia wadogo kwa wakubwa, wala sisemi neno ila yale ambayo manabii na Musa waliyasema(m.22). Roho Mtakatifu ndiye aliyemwongoza hata katika kusema na mfalme Agripa. Yesu alitimiza ahadi yake kwake (Mt 10:18-20, Mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu). Habari ya Injili ni habari ya ajabu sana, ni ujumbe usiowahi kusikika duniani. Kwa hiyo kuna mawili: 1. Watoao habari hii wana wazimu. Yaani haina ukweli ndani yake (ling. m.24:Festo akasema kwa sauti kuu, Paulo, una wazimu, kusoma kwako kwingi kumekugeuza akili). 2. Habari hii ni kweli, na kama ni kweli lazima watu watubu na kumwamini Yesu (ling. m.28: Agripa akamwambia Paulo, Kwa maneno machache wadhani kunifanya mimi kuwa Mkristo– au kama ilivyotafsiriwa katika Biblia Habari Njema: Kidogo tu utanifanya Mkristo).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz