Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 7Mfano

Soma Biblia Kila Siku 7

SIKU 24 YA 31

Paulo hakutaka kwenda kuhukumiwa Yerusalemu. Alijua Wayahudi walitaka kumwua tu. Tena alijua kwamba Yesu amepanga aende Rumi: Paulo akaazimu rohoni mwake, akiisha kupita katika Makedonia na Akaya, aende Yerusalemu, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi pia(19:21). Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako(23:11). Kwa hiyo akaamua kukata rufani kwa Kaisari yaani kiongozi mkuu wa taifa la Warumi. Aliweza kufanya hivyo kwa sababu ni raia wa taifa hili yaani ni Mrumi. Hapa tujifunze kwamba tusikubali mateso na kifo kwa ajili ya jina la Yesu ikiwa sheria na kanuni za taifa zinatulinda. Kama tunaweza kujitetea kutokana na sheria basi tujitetee tukisema ukweli mtupu – kama Paulo anafanya katika m.11: Ikiwa ni mkosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; bali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezaye kunitia mikononi mwao. Nataka rufani kwa Kaisari.

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 7

Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz