Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
Na Paulo alipokuwa akitoa hoja zake katika habari ya haki, na kuwa na kiasi, na hukumu itakayokuja, Feliki akafanya hofu akajibu, Sasa enenda zako, nami nikipata nafasi nitakuita (m.25). Feliki alipoguswa moyoni mwake na ujumbe wa Paulo akakatisha mazungumzo mara. Ndivyo ilivyo hata leo. Wengine wanaposikia Bwana anagonga mlango wa mioyo yao huzidi kufunga mlango kwa nguvu badala ya kumfungulia! Nikipata nafasi, neno hili linakemewa na Waebrania 4:7, Leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu!Zingatia pia Isaya 55:6-7, Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz