Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutafuta AmaniMfano

Finding Peace

SIKU 1 YA 17

Msingi wa Amani yote

Kabla ya tukio la mkutano muda si mrefu uliopita, mfanyakazi wangu na mimi tulikuwa tunafurahia chakula katika pwani ya magharibi. Wakati muhudumu binti mdogo akituhudumia mezani kwetu wakati wa chakula, nilimuuliza: " Kama ungemuomba Mungu chochote maishani mwako, ungemuomba akufanyie nini?"

Pasipo kusita, alijibu: " Ningemuomba amani." ”

Machozi yalianza kutiririka wakati akitusimulia juu ya kifo cha bibi yake mpendwa siku chache zilizopita.

Alipokuwa anasimulia hadithi yake, niliona kwamba hakuna anayemwamini Mungu katika familia yake--wala yeye mwenyewe. Hakumkataa Mungu kwa kujua. Kitu alichojua ni kwamba kulikuwa na mahangaiko mengi ndani yake, lakini alikuwa hana uelewa juu ya namna ya kutuliza huo mtikisiko wa ndani, au hata kilichokuwa juu yake. Kama walivyo watu wengi, alikuwa anaishi siku baada ya nyingine, pasipo kuwa na makusudi au maana katika maisha yake.

Huyu binti anawakilisha watu wengi katika jamii yetu leo--wakienda kwa misukumo, wakijitahidi kusogeza maisha, wakitafuta njia pasipo kuwa na njia, na wakijaribu kutafuta maana ya yote hayo.

Mara nyingi, inaonekana hakuna majibu ya kutosha kwa shida za wanadamu-- hasa kwa swali la kwa nini tunajisikia watupu, wazi, na kukosa amani. Zaidi, kunaonekana hakuna sababu ya kutosheleza ya sisi kuendelea kuweka juhudi na bado tunateseka na magumu ya maisha.

Yule binti aliyekuwa akituhudumia alieleza jambo katika msemo wake kwa kusema, " Nataka amani." Wengine wangesema " Niko mpweke." Wengine wangesema, " Kama mwenzi wangu angenipenda kama anavyotakiwa, basi ningekuwa na furaha." Maneno tofauti lakini sauti ileile: " Kuna tatizo mahali... sina furaha. Sina amani. Nina shida gani?"

Wengi ambao ni wahanga wa jumbe za jamii yetu wanapata utupu huu na hawahusishi matatizo yao na Mungu. Mara zote tunapigwa na madai ya jamii: " Kama tuu ungekuwa mwembamba, ungevaa nguo za mitindo zaidi, ungeendesha Jaguar, ungeishi sehemu maarufu mjini, ungekuwa na fedha nyingi..." orodha inaendelea. Lakini hakuna moja kati ya hayo majibu au mamia ya majibu mengine tunayopewa yanaweza na kwa utoshelevu kutupa kile ambacho tunakitamani sana.

Yule binti alisema vizuri: wengi wetu kwa uhakika tunahitaji kitu zaidi--na neno moja linalojumuisha vyema na kuelezea ni amani.

Na kama mchungaji kwa zaidi ya miongo sita, naweza kukwambia kwamba ni mpaka utakapokuwa na amani na Mungu, hutaweza kupata amani ya kweli katika maisha yako.  

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Finding Peace

Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.

More

Tungependa kushukuru In Touch Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://intouch.cc/peace-yv