Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutafuta AmaniMfano

Finding Peace

SIKU 4 YA 17

Vitu 5 vya imani kwa Moyo wenye Amani

Kama wewe ni mkristo, Mungu pekee ndiye mwenye mamlaka ya maisha yako. Yeye ndiye usalama wako. Na hajawahi kuacha kuongoza maisha ya uumbaji wake hata kwa sekunde moja toka kuumbwa kwa ulimwengu. Hajapoteza hata mamlaka kidogo. Yupo kila mahali, anajua yote, ni muweza wa yote, na mwenye upendo leo kama alivyokuwa wakati wa anguko la mwanadamu.  

Japokuwa tunaweza siku zote kuelewa kusudi lake, kuzielewa njia za Mungu siku zote hupelekea kuelewa kwamba hufanya kazi katika njia ambayo huleta amani ya milele kwa watoto wake. Kwa miaka yote, nimegundua imani muhimu tano kwa ajili ya moyo wenye amani. Nakupa changamoto chukua muda, zingatia kile unachoamini kuhusu Mungu. Amani yako inapimwa kwa kiwango ambacho kweli hizi zimo ndani ya moyo wako.

Imani 1: Mungu ana uhuru.
Kutambua na kukubali kweli kwamba Mungu yuko huru juu ya kila kitu muhimu kwa ajili ya amani yako. Hii ina maana hakuna kinachohusiana na wewe kiko nje ya jicho lake la uangalizi wake na upendo wake. (Kolosai. 1:17)
Imani 2: Mungu ni mpaji wako.
Kutoka mwanzo mpaka mwisho, Biblia ina ujumbe wa wazi kwamba Mungu ndiye atupaye mahitaji yetu. Hakuna mahitaji yaliyo makubwa, magumu, ambayo Yesu hawezi kutimiza. Biblia inatuambia, “Bali wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu" (Zab. 34:10).
Imani 3: Mungu alikuumba jinsi ulivyo kwa kusudi.
Kuna mambo mengi ya maisha yako ambayo huna mamlaka nayo. Yakubali mambo hayo kama sehemu ya jinsi Mungu alivyokuumba. Rangi yako, mila, lugha, utaifa, jinsi, na sifa nyingine nyingi za utu wako kama "mapenzi" ya Mungu. Pia alikupa karama, vipawa, akili, utu, na karama za kiroho ambazo, zinachukuliwa kwa ujumla wake, kukufanya wewe kuwa mtu tofauti hapa duniani kutimiza mpango alionao kwako. (Zab. 139:13-16)
Imani 4: Mungu ana nafasi mahali unapostahili.
Mungu alikuumba wewe kwa ajili ya ushirika na yeye na wengine. Mwamini kukusaidia kupata hali ya kuwa mali yake na kukupa "familia" ya waamini wenzako ambao unakuwa sehemu yao. Ndipo, unapokua ndani yake, wafikie na wengine. (1 Pet. 2:9).
Imani 5: Mungu ana mpango kwa ajili ya utimilifu wako.
Kwa amani ya kweli, mtu anahitaji kujua kwamba ana sifa, anaweza, na ana ujuzi katika kufanya kitu. Kuna kujisikia amani kwa ajabu inayopatikana unapojua kwamba unaweza kufanya kitu vizuri zaidi. (Ef. 2:10)

Unapokubali mahitaji haya matano ya imani kwenye kilindi cha utu wako na kuamini kwamba Mungu anafanya ndani yako na kwa niaba yako, amani ya ndani hakika itakuwa yako.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Finding Peace

Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.

More

Tungependa kushukuru In Touch Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://intouch.cc/peace-yv