Kutafuta AmaniMfano
Kuacha Wasiwasi
Wasiwasi ni tatizo ambalo wote tutashughulika nalo wakati fulani. Katika hotuba ya mlimani, Yesu alisema:
Kwa sababu hiyo nawaambieni, msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini, wala miili yenu, mvae nini. Maisha je, si ni zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba, hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani, na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? (Mathayo. 6:25-26)
Neno la kiyunani la "wasiwasi" katika kifungu hiki humaanisha " "kuondoa usikivu". Ni neno linaloonesha kutokuwa na uhakika. Na ndicho wasiwasi unachotuletea ndani yetu. Unatupa kujisikia Nini kifuatacho? Ni kujisikia kwamba zulia limeondolewa chini yetu na hatuna uhakika kama tutaanguka, kiasi gani,na kwa mwelekeo upi, au juu ya nini.
Neno "wasiwasi" limetafsiriwa kama " mashaka" katika Biblia. Kwa watu wengi, mashaka yamekuwa mfumo wa maisha. Kama hilo linakuelezea wewe, nakutia moyo usome tena maneno ya Yesu. Maneno yake siyo mapendekezo-- ni maagizo.
Unaweza kusema, " Siwezi kujizuia kuwa na wasiwasi, siku zote nimekuwa mtu wa mashaka." Nimesikia hivyo kutoka kwa watu wengi miaka yote. Majibu yangu yamekuwa, " Ndiyo unaweza".
Hakuna kitu kama mazingira ambayo yanaleta wasiwasi. Wasiwasi unatokea kwa sababu ya namna tunavyopokea matatizo au hali ya shida. Uwezo wako wa kuchagua ni sehemu ya karama yako ya bure ya Mungu kwa kila mwanadamu. Unaweza kuchagua unavyojisikia. Unaweza kuchagua kile unachokifikiria, na unaweza kuchagua jinsi utakavyoitikia katika mazingira fulani. Ni wazi siyo kusudi la Mungu kwako kuwa na wasi wasi-- Haruhusu mazingira fulani maishani mwako ili uwe na wasi wasi. Baba anaweza kuruhusu mazingira fulani maishani mwako ili kujenga imani imara, kukua na kukomaa, kubadilisha tabia mbaya au mtazamo hasi. Lakini Mungu hakuletei wasiwasi. Siku zote yuko kazini kukuleta mahali utakapomwamini zaidi, kumtii zaidi, na kupokea baraka zake zaidi.
Unaweza kuanguka kwenye gurudumu la wasiwasi. Au unaweza kusema, " Baba nalileta hili kwako. Ni zaidi ya uwezo wangu. Najisikia kukosa msaada katika hali hii, lakini wewe una nguvu za kubadilisha nachokabiliana nacho. Unanipenda sana, na mimi nakutumaini kuhusika na linalonihusu kwa namna uonavyo sahihi. Najua chochote ulichokipanga ni chema kwangu. Nakutazamia kuona jinsi utakavyoonesha upendo wako, hekima na nguvu."
Rafiki, hii ndiyo njia ya amani--barabara ya kutoka kwenye wasiwasi na mashaka.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.
More