Kutafuta AmaniMfano
Kushinda Hofu
Watu wengi wanadhani kinyume cha hofu ni tumaini, ujasiri, au nguvu. Kinyume halisi cha hofu ni imanifaith. Na wakati hofu inapoleta kupooza, siyo tuu inazima amani ya mtu, lakini pia inashambulia msingi wa amani hiyo- unaoitwa, imani yetu. Amani hutokea dirishani kunapokuwa na hofu.
Hofu nyingi msingi wake ni mashaka kwamba Mungu atakuwepo, atatoa haki au msaada, au kuweza kushughulika na tatizo lililopo. Imani inasema, "Ndiyo, Mungu yupo hapa. Ndiyo, Mungu atatoa. Ndiyo, Mungu anaweza mambo yote!"
Hofu nyingi chanzo chake ni vitisho-wakati mwingine maneno ya vitisho, wakati mwingine tabia za vitisho. Imani inasema, " Sitatishwa na vitisho. Nitatenda kwa hekima, si kwa kuhofia. Naamini Mungu atazuia vitisho vyote kuja kwangu kutokea. Na kama vitisho vikitokea, naamini Mungu atanisaidia kushughulika na chochote nitakachotupiwa.
Wakati Sauli, mfalme wa Israeli, alipotambua kwamba Mungu ameondoa mkono wake wa upako na baraka kwake ( kwa sababu ya kiburi chake na kutokutii kwake) na badala yake ameweka juu ya kijana mdogo, Daudi, alikasirika. Alianza kampeni ya kumtafuta Daudi na kumuua-kuondoa kitisho katika maisha yake ( 1 Samweli 19). Kwa upande mwingine, Daudi alijisikia kutishiwa na jeshi la Sauli na mara kadhaa aliogopa juu ya uhai wake. Lakini maandiko yanatuambia kwamba Daudi alitiwa nguvu na ahadi za Mungu kumlinda na siku moja kumfanya mfalme wa Israeli.
Katika ulimwengu wetu wa sasa, mara nyingi tunasoma juu ya watu ambao, pamoja na vitisho vya magonjwa, ajali, au hatari, walisonga mbele kwenye matokeo yasiyo na uhakika- kukataliwa, kushindwa, na, ndiyo, wakati mwingine ushindi. Wavumbuzi wa Arctic, Wanariadha wa Olimpiki, wamisionari, watu wa mitaji, na wavumbuzi huja akilini. Kwa hiyo vitisho havitakiwi kutulemaza.
Changamoto yetu wakati wa vitisho si kuangalia Vinavyowezakuwa halisi, bali, kutazama kile tunachoweza kuhesabu kwamba ni kweli.
Watu wengi wanaishi chini ya wingu jeusi la kitisho leo. Wengine wanapitia kitisho cha ugonjwa, wengine wanakabiliana na kitisho cha kuumia watoto wao, na wengine wanasikia vitisho vinavyohusiana na kupoteza kazi zao.
Jibu la vitisho vyote hivi ni imani juu ya kile tunachokijua kuwa kweli kuhusu Mungu na kuhusu upendo wake na uangalizi wake kwetu na uwezo wake wa kukutana na mahitaji yetu- hasa amani yake, ambayo inaweza kutupitisha.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.
More