Kutafuta AmaniMfano
Kuishi kwa Amani na Wengine
Ni changamoto ambayo wote tunakabiliana nayo mara nyingi: Tunawezaje kuishi kwa amani na watu wengine na kurejesha amani wakati ugomvi unaibuka?
Ukweli ni kwamba, Mungu anatamani tuishi kwa amani na wengine. Ugomvi hutokea. Wakati mwingine ugomvi hauishi kirahisi. Ukweli, kuna nyakati ambapo ugomvi hauwezi kumalizwa. Hata hivyo, Mungu anataka tufanye tuwezavyo kuwa na amani na kila mtu.
Sisi tulio wafuasi wa Kristo tunajua wazi kwamba Mungu asipotawala maisha yetu, tunaweza kuishi kwa kudharauliwa kama wasioamini. Wokovu wetu hautukingi na kuwa wachoyo, wenye wivu, wenye chuki, au wenye kukasirika. Ni pale tunapomuomba Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yetu na kupitia kwetu, tunaposalimisha asili yetu kwenye asili yake, tunapotafuta kuwa wawakilishi wake hapa duniani katika kila uhusiano tulionao na kuenenda zaidi ya fahari yetu kuelekea tabia itakayoleta amani.
Tunashughulikaje na ugomvi unapotokea na kuleta matokeo ya amani?
Kwanza, angalia thamani ya uhusiano. Kama unataka kuishi kwa amani na mtu mwingine, yakupasa kuamua, "Uhusiano huu ni wa thamani sana kuutunza? Je, niko tayari kuelewana katika mambo fulani ili uhusiano uendelee?” Ninaamini hakika wale waliookolewa kwa neema na Roho Mtakatifu yuko ndani yao wanaweza kupata amani halisi katika uhusiano wao wakati wote wanapothamini kuutunza.
Pili, anza kuongea... na endelea kuongea. Wakati watu wawili wanapoongea--na wako tayari kuendelea kuongea na kusikilizana---wanaweza kupata suluhisho la ugomvi wao na kuishi kwa amani kila mtu na mwenzake.
Tatu, kuwa muwazi. Huwezi kuwa na jambo umelificha au mpango wa kumzunguka akilini mwako na kutegemea kuwa na uhusiano wa amani. Kuwa muwazi na mkweli kwa kila mmoja wakati ugomvi unapotokea huwasaidia kufikia suluhisho la amani kwenye uhusiano wenu.
Mwisho, nenda kwenye kiini cha tatizo. Unapowasiliana kwa uwazi na wengine, na kuchukua mtazamo wa wazi juu ya kiini cha tatizo, utaweza kufanya kazi katika magumu hayo na kuleta amani.
Unapojitahidi kuishi kwa amani na watu, ukisimama katika kweli ya neno la Mungu, jua kwamba Mungu anasimama na wewe. Atabadilisha kila ugomvi au mateso unavyopitia kwa faida yako ya milele. Ataleta kukua kiroho, imani kubwa, na uwezo mkubwa wa kuhimili ndani yako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.
More