Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutafuta AmaniMfano

Finding Peace

SIKU 10 YA 17

Kujifunza kuishi kwa utoshelevu.

Kuishi kwa utoshelevu wa ndani, mtazamo mzima wa maisha yako lazima uwe ni Bwana Yesu Kristo.  

Nimekuwa na vipindi fulani katika maisha yangu wakati tatizo fulani lingenisababishia usiku wa mahangaiko, saa baada ya saa, na kukosa usingizi. Nimegundua kitu kilicho bora naweza kufanya wakati inaonekana siwezi kuacha kufikiria juu ya tatizo fulani, mazungumzo, au shutuma, ni kutoka kitandani, kupiga magoti, kumlilia Mungu: Tafadhali nisaidie katika hili. Nisaidie nikutazame wewe tuu.”

Usingizi huja wakati namwangalia Bwana na jinsi atakavyo nifanya nifikirie au majibu ya hisia zangu juu ya mazingira fulani. Usingizi hupotea wakati naporuhusu mtazamo wangu kuhama na kusikiliza watu walichosema, mambo yote yanayoweza kutokea, au ugumu wa changamoto iliyo mbele yangu. Uchaguzi ni rahisi tu--fikiria juu ya Bwana na utoaji wake, ulinzi, na upendo, au fikiria juu ya watu wote na mazingira vinavyojaribu kuiba vitu vyako, kuharibu maisha yako, au kuchochea chuki dhidi yako.

Kufikiria juu ya Bwana humletea mtu amani. Kufikiria kitu kingine chochote ni njia fupi kuelekea kuwa na wasiwasi, hofu, au mashaka.

Unapomtazama Bwana, ni muhimu kwamba unamuona kama yuko kwenye hali yako pamoja nawe, wakati uleule. Watu wengi wanafikiria Mungu yuko mbali sana. Hawamuoni Mungu kama anapatikana kwao katika harakati ya maisha yao. Ukweli ni kwamba, yuko pamoja nasi nyakati zote za siku.

Naweza kukumbuka sehemu yenye amani ambayo nimewahi kuwa--bahari ya Galilaya. Miaka iliyopita, nilikuwa eneo ambalo kwangu ni kama kielelezo cha amani na utulivu. Hata hivyo, katika dunia ya sasa, watu wengi hawawezi kufikiria eneo hilo kuwa lenye amani. Ni maili chache tuu kwenda Syria na Lebanoni kutoka hapo. Watu hufikiria juu ya Israeli kama eneo hatari ulimwenguni, na ni mahali pasipo na amani kabisa.

Lakini nilipata amani sana pale. Kwa nini? Kwa sababu nilimhisi Bwana pale. Nilihisi uwepo wake.

Ni rahisi kwangu kufumba macho na kumuona Bwana akitembea nami pembeni mwa bahari ya Galilaya. Pia naona rahisi na faida kufikiria Bwana anatembea nami katika sehemu nyingi za mazingira asili niliyotembelea ulimwenguni.

SiyoMazingira hayayanayoleta amani. Ni ufahamu wa Mungu naouhisi moyoni mwangu ninapokuwa kwenye mazingira haya unaoleta amani. Katika hisia hiyo ya "Mungu kuwa nami" ni muhimu kwangu kurejea, kupata picha, kuona kwa macho ya kiroho, wakati nyakati za shida zinapokuja maishani mwangu.

Rafiki, haijalishi uko wapi wakati wowote, Yesu ndiye chanzo cha utoshelevu wako. Muone Bwana akitembea nawe kwa amani. Hisi uwepo wake. Ujue nguvu yake ya ajabu na mamlaka yake juu ya maisha yako. Wakati kwa imani unaingia katika uhusiano binafsi na Kristo, kuishi kwa uhakika wa uweponi mwake na utoaji wake katika maisha yako, nakuahidi utapata amani ya kweli.


Kama unashindana na tetemeko katika ulimwengu usiokuwa na uhakika, bofya hapa kujifunza zaidi jinsi unavyoweza kupata na kuishi kwa amani.

­

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Finding Peace

Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.

More

Tungependa kushukuru In Touch Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://intouch.cc/peace-yv

Mipangilio yanayo husiana