Kutafuta AmaniMfano
Kuishi Bila Majuto
Nakumbuka kukata simu taratibu na kusema wakati napumua kwa nguvu, "Sawa… imetokea.”
Sauti upande mwingine wa simu alikuwa ni hakimu, akiniambia mke wangu amefungua kesi ya talaka.
Nimeishi na vitisho vya talaka kwa miaka mingi. Hata hivyo, nilistushwa na habari hizo nilizopewa.
Zaidi ya siku kadhaa zifuatazo, fikra mbalimbali na mawazo vilipita moyoni mwangu na kichwani mwangu. Sikutaka talaka. Sikujua hasa jinsi ya kuendelea kuzuia talaka kutoka. Sikujua wa kumwambia, na nimwambieje. Nilijua hatimaye kuwa nitahitaji kuwaambia washirika wote wa kanisa nililokuwa nachunga, na sikuwa na uhakika jinsi gani bodi ya kanisa au washirika watalipokea. Uhakika pekee ulikuwa ni shinikizo la kuandaa na kuhubiri katika ibada ya jumapili inayofuata.
Hata mawazo yangu yalipokuwa yanakwenda maili milioni moja kwa sekunde, nilijua kwa uhakika kabisa ndani ya moyo wangu kweli hizi:
· Mungu hakushangazwa na hatua hii iliyochuliwa kinyume nani.
· Mungu alikuwa anatawala maisha yangu---Aliruhusu hili kutokea kwa kusudi lake kama sehemu ya mpango wake kwangu.
· Ameahidi katika neno lake kutoniacha wala kunipungukia. Aliahidi kuwa karibu katika kila hatua ya njia yangu; na kwa hiyo, mambo yote yatakuwa kwa faida yangu milele kama tuu nitaendelea kumwamini yeye kikamilifu.
Ukweli wa ghafla wa hali yangu ulizua mtafaruku. Ukweli usiobadilika kuhusu Mungu ulileta amani.
Karibia miaka nane toka hakimu anipigie simu, talaka mke wangu aliyotaka ilitolewa kisheria kwake.
Watu wameniambia miaka hiyo yote: Hakika utakuwa unajutia kupoteza ndoa yako… kwamba ulishindwa katika kupambana kuinusuru ndoa yako … kwamba juhudi zako kupatanisha hazikuzaa matunda.”
Majibu yangu siku zote yamekuwa kunyamaza tuu. Majibu yangu kwa maneno hayo ni Nimestushwa, ndiyo. Nasikitika, hapana.
Nikiwa nimestushwa kwamba ndoa yangu inaishia kwenye talaka, siishi na hali ya kujuta. Kwa nini? Kwa sababu majuto yanatokana na hukumu isiyo na ufumbuzi. Nilijua nilikuwa na amani na Mungu, na majuto na hukumu siyo sehemu ya maisha yangu.
Nimepata njia bora ya kuishi bila majuto ni kuwa na dhamiri safi. Chagua kuishi kwa namna ambayo unafanya vizuri katika kila jambo na uhusiano wako, ukijitahidi kuishi kimungu. Chagua kumwamini Mungu katika kila eneo la maisha yako—na siyo yaliyo rahisi. Chagua kumtii na kushika amri zake. Chagua kusamehe wengine kikamilifu. Na chagua njia Mungu anayokuonesha ili uifuate.
Wakati hakuna anayeweza kufanya yote haya kwa nguvu zake, tukiwa na Roho Mtakatifu akikaa ndani yetu, tunaweza kutoka kwenye aina zote za majaribu ili kutafuta amani sisi wenyewe na wengine--na kuendelea kazi nzuri ya Mungu aliyoruhusu kwa ajili yetu kufanya.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.
More