Kutafuta AmaniMfano
Jinsi Maisha ya Mawazo yako yanaathiri Amani yako
Kama tunakuwa wa kweli kwetu wenyewe, wengi wetu hatuko vile tunavyodhani tuko. Mawazo yetu yako nje ya mstari, na mara nyingi, yanahitaji kubadilishwa.
Najuaje kwamba hili ni kweli? Mbali na uzoefu wangu wa kuwa mchungaji wa watu wengi miaka mingi, Neno la Mungu linatutaka "kuyafanya upya" mawazo yetu. Hii ina maana kwamba kutenda kutumia uelewa, mawazo, maoni, imani na tabia zetu za kujiamini kwa zamani kwa ajili ya seti mpya ya uelewa, mawazo, maoni, imani ambao Mungu anauweka ndani yetu. Muitikio huu wa kimungu unakuzwa na usomaji wa maandiko na kutafakari kwa kile ulichokisoma katika Biblia. Wafuasi wa Kristo wanatakiwa kujizuia "kufuata namna ya dunia hii, bali wageuzwe kwa kufanywa upya nia zao, wapate kujua yaliyo mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” (Rum. 12:2).
Kutokana na kufanywa upya mawazo yetu huja mabadiliko katika mfumo wa kauli zetu na tabia zetu. Wakati kauli zetu na tabia zetu zinapofanywa upya, uhusiano wetu na wengine unafanywa upya. Na wakati uhusiano wetu unapofanywa upya, na ulimwengu wetu wa karibu unabadilishwa pia. Yote yanaanzia na nia zetu kile tunachochagua kuwaza na tunachochagua kukifuata.
Una uwezo wa kuamua kitu gani utakachofikiria. Kwa wakati wowote, unaweza kugeuza nia yako kwa kitu kipya, kazi mpya, au tatizo la kutatua badala ya mawazo hasi kwamba litaiba amani yako na/au kukufanya kuingia kwenye uasi au dhambi. Unao uwezo wa kusema, "Nachagua kumwamini Mungu," katika hali yoyote unayokabiliana nayo au unayofikiria unayo.
Tena, kila mtoto wa Mungu anayeamua kuchukua msimamo wa hiari kusimama kinyume mifumo ya mawazo ambayo ina athari itatoa njia ya kutoka katika mazingira hayo. Mungu atakusaidia kuweka mawazo yako kwenye kitu kingine kuliko matatizo yako, mfumo wa mawazo mabaya kama utachukua hatua kwenye uongozi wake.
Unapochunga mawazo yako, unachunga amani yako. Unapofanya maombi kwa Mungu kwa imani na shukurani--haijalishi majaribu gani unapambana nayo--anakuhakikishia amani ya ndani (Wafil. 4:6-7). Na unapoweka mawazo yako kwenye kitu ambacho ni kweli, staha, haki, kupendeza, safi, sifa njema unamtegemea Mungu kwa imani na tumaini zaidi.
Hutaweza kamwe kumaliza uwezo wako wa kuwaza juu ya wema na ukuu wa Mungu. Chagua kufanya katika maisha kama Yesu alivyofanya. Chunga maisha yako ya maombi. Chunga mawazo yako. Mtafute Baba na kila lililo la kimungu. Neno lake linaahidi kwamba unapojaza na kile ambacho ni staha na sifa njema, "Mungu wa amani atakuwa pamoja na wewe" (Wafil. 4:9).
Kuhusu Mpango huu
Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.
More