Kutafuta AmaniMfano
Kwa nini Tunapoteza Amani Yetu
Kuna njia moja tu ya kupata amani idumuyo ipitayo mazingira yote--kwa imani. Imani ni msingi wa kuishi katika amani ya Mungu--itendayo, tumaini la uhakika katika uwepo wake na nguvu yake kuendelea na kukufariji, pasipo kujali mazingira unayokabiliana nayo. Ingawa, kuna mambo fulani yanayoweza kushusha imani yetu na kuiba imani yetu. Hebu tuangalie vichache:
1. Hofu ya ghafla—Baadhi ya watu wamezoea kujibu kila shida ya maisha kwa hofu na kuchanganyikiwa kidogo ambako hakuwezi kuelezeka kwamba kuna njia nyingine ya kujibu. Wanakasirishwa na mabadiliko yoyote ambayo hayawezi kuwaangusha na wanaweza kuishi kwa hisia thabiti.
2. Adui—Tunaweza kushambuliwa na adui wetu, shetani, ambaye anaweza kutumia njia mbalimbali kututia mashaka na kupoteza imani kwa Mungu wetu. Lakini lazima tusimame na Mungu. Maandiko yanatutaka tumpinge shetani, na tukifanya hivyo, atatukimbia. (Yakobo 4:7).
3. Dhambi—Amani na uasi haviwezi kukaa pamoja. Njia pekee ni kuungama dhambi zetu kwa Mungu, kujisalimisha kwake, na kuomba msaada wake ili kuokoka na kushinda majaribu yote. Ndipo, Amani ya Mungu inaweza kurejea tena.
4. Kupoteza Imani—Nyakati za shida, wakati mwingine tunatupa amani yetu kwa hiari. Tunakata tamaa. Tunakubali kushindwa. Tunaacha. Siku zote kumbuka kwamba hakuna mtu anaweza kuchukua amani yetu; tunaisalimisha. Kwa namna hiyo, sisi ndiyo pekee tunaoweza kuirejesha.
5. Kupoteza uzingatiaji—Tunaweza kuruhusu matukio mengi ya habari mbaya tunazosikia au kusoma kila siku kutufanya kupoteza uzingatiaji. Badala ya mawazo yetu kuzingatia Mungu na kumwamini kwa ajili ya amani yake na uwepo wake, tunaruhusu mawazo yetu kupotoshwa na kujawa na taarifa hasi na mazingira tunayoyaona na kusikia.
Kwa sababu Mungu yupo pamoja nasi, hatuhitaji kukubali, kuzama chini, au kushindwa na matatizo yetu. Tunaweza kukabiliana, kupambana, kushughulika, na mwishowe kuyashinda kwa nguvu ya msalaba. Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kwamba matatizo yanapita na majira yake … na sababu yake. Kwa hiyo, “msisumbuke mioyoni mwenu” (Yohana 14:27). Shikilia amani ambayo Mungu anakupa, ukiwa na ujasiri kwamba anaangalia, anaongoza, na kujali wale wanaomtumaini na kumwamini.
Kuhusu Mpango huu
Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.
More