Kutafuta AmaniMfano
Amani atoayo Mungu
Kama wewe ni mwanafunzi wa Biblia, nina uhakika umegundua kwamba mtazamo wa Mungu mara nyingi unatolewa kwa namna ya kulinganisha na kutofautisha. Kwa mfano, mara nyingi alilinganisha tajiri na maskini, wenye hekima na wapumbavu, giza na nuru,na kuhusiana na mada yetu, amani itokayo kwa Mungu ni tofauti na amani inayopatikana katika ulimwengu huu. Yesu alisema, " Amani yangu nawapeni, lakini si kama amani ya ulimwengu itoayo...." (Yohana 14:27).
Ni wazi, Bwana alikuwa anaeleza kwamba amani aliyowapa wafuasi wake ilikuwa tofauti na amani wanayoweza kuipata ulimwenguni. Yesu aliposema "ulimwengu", alikuwa anazungumza kwa jamii na utamaduni ambao wanadamu wanaishi.
Je umewahi kuwa katika bahari iliyochafuka? Nimewahi kupata dhoruba baharini mara nyingi na kusema kweli, nisingependa kurudia hali hiyo tena! Nchi kavu, upepo unaweza kuvuma baharini kwa kasi ya maili 40, 60, 100 kwa saa, kukiwa na mvua, radi, ngurumo, na giza nene. Mawimbi yanaweza kuinuka futi 20, 30, hata 50 juu. Meli katika hali kama hiyo inaweza kusukwa sukwa kama mtumbwi wa kuchezea watoto. Ni rahisi kwa chombo hicho cha baharini kupotea katika dhoruba hizo. Lakini chini ya kilindi, kama futi 100 chini, hakuna dhoruba. Kuna utulivu mkubwa. hakuna sauti. hakuna usumbufu. Hata chembe ya dhoruba.
Huu ukweli unafanya nifikirie amani ya Mungu. Inanipa ufahamu wa kile alichokuwa anasema Bwana wetu alipokuwa anawaahidi wanafunzi wake amani. Aliwaambia kwa sababu walikuwa wanafunzi wake, walikuwa na matatizo katika ulimwengu huu. Na kweli, alisema kwamba wengine watateswa kwa sababu ni wanafunzi wake. Lakini pamoja na hayo, aliahidi kwamba hatawaacha wale wanaomfuata, na uwepo wake utakuwa ndiyo njia watakayopata amani yake.
Wakati hofu, mashaka, na shida zinapoinuka katika maisha yako, angalia ishara zifuatazo za amani ya Mungu kama ilivyo...
· Hupita hali zote. Mara nyingi, amani inaonekana haraka na kuonekana katikati ya majaribu na shida. Lakini pasipokujali unapitia hali gani, jua hili: Mungu ndiye amani yako. Weka imani yako kwake.
· Hupita ufahamu wote. Amani ya Mungu siyo kitu ambacho unaweza kukifikiria. Lakini hufanya kazi na inapatikana kwetu-zaidi ya uwezo wetu wa kueilewa.
· Inatolewa kwa wafuasi wake wote. Amani ya Mungu inatolewa kwa kila mtu anayempokea Yesu kama mwokozi wake, anayeziacha dhambi zake, na kuishi maisha ya utii kwa uongozi wa neno la Mungu na Roho Mtakatifu.
· Ni hali ya utu ikaayo .Katika nyakati ngumu za maisha, Roho Mtakatifu yupo kutoa msaada. Amani--ya ndani, ya kweli, inayotolewa na Mungu--inaweza kuwa ni desturi yako ya kila siku.
Unapoendelea mbele na safari ya maisha, amini na kubali kwamba nia ya Mungu juu yako ni kusikia amani ikaayo wakati wote--amani inayojumuisha furaha na kuhisi kusudi katika maeneo yote ya maisha.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.
More