Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mazungumzo na MunguMfano

Conversations With God

SIKU 6 YA 14

Sauti ya Bwana mara nyingi siyo kubwa. Roho mtakatifu mara nyingi hunong'oneza. Katika nyakati ambazo anaonyesha kujali, ni jambo jema kujitenga na uwezekano wa mtego. Vilevile, anapoonesha baraka, tunaweza kuamua kutii na kuchukua nafasi hiyo kwa imani. Bwana si kila mara anarudia, kwa hiyo lazima tuwe wasikivu kwa sauti yake na kutenda. 

Mchana mmoja katikati ya kiangazi, nilipokea msukumo ambao ulibadirisha muelekeo wangu. Wanangu wengi wamekuwa wakisoma shule moja ya kikristo katika eneo letu. Mjumbe wa Bodi, ambaye pia alikuwa rafiki, alipiga simu kuuliza kama naweza kuhudhuria usaili kwa ajili ya nafasi ya mkufunzi wa uandishi kwa ajili ya muhula ujao wa shule.

Ni hisia ya namna gani ya kutokutarajia. Nakumbuka vyema jinsi inavyotumia akili na kuweka sawa kulikofanyika nyuma ya maongezi hayo ya simu. Kwanza kilichokuja ni kinyume: nilikuwa na shahada ya maarifa. Nilijua kidogo sana juu ya uandishi wa makala. Sijafanya kazi nje ya nyumbani kwangu kwa miaka mingi. Kufundisha madarasa nje ya nyumbani kwetu kungeathiri taratibu za famila yetu. Nafasi hii ilihitaji kazi nyingi. Sikuweza hata kujua naanzia wapi. Na kwa nini nifikirie kwamba nitaajiriwa kushinda waalimu wengine wenye sifa zaidi wanaosailiwa kwa ajili ya hiyo nafasi?

Baadaye likaja wazo la kuwezekana: Je, kama hii ilikuwa ni nafasi ya kufidia gharama ya ada? Hata kipato kidogo kingebariki bajeti ya familia. Zaidi, nilipenda kufundisha na ni mzuri katika hilo. Nafasi ya kufundisha nje ya nyumbani kwangu ingekuwa ni changamoto nzuri! Kama Mungu angenichagua kwa ajili ya nafasi hii, hekima yake na nguvu zake zisingeenda na wajibu huu? 

Katikati ya mchanganyiko huo, Bwana alinena. Ilikuwa kana kwamba mkono wake kauweka begani kwangu--mara moja tuu lakini kwa utaratibu. Ilikuwa hivyo tuu. Alionesha kwamba kufanyiwa usaili kwa nafasi hii ilikuwa ni njia ya baraka. 

Niliajiriwa ndani ya mwezi mmoja. Ndani ya miezi miwili Bwana alinifunilia maono ya kazi. Baada ya miezi mitatu, nilikuwa naandaa mtaala, nakutana na wanafunzi, na kushangaa-- nikifurahia kila hatua. Sasa najua kwamba pasipo hii changamoto, nisingepata ujuzi na ujasiri wa kuandika kitabu kuhusu maombi kilichofuata. Baraka zimekuwa nyingi kwa ajili ya hatua hii moja ya utii. 

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Conversations With God

Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!

More

Tunapenda kumshukuru Susan Ekhoff kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.amazon.com/Prayer-That-Must-Power-Conversational/dp/1496185560/ref=sr_1_1?ie=UTF8&qid=1498693709&sr=8-1&keywords=prayer+that+must+the+power+of+conversational+prayer