Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mazungumzo na MunguMfano

Conversations With God

SIKU 11 YA 14

Maandiko yameonesha nyakati nyingi za mtazamo wa Bwana na maelekezo yake kupitia ndoto. Angalia Yakobo, Yusufu ( mwana wa Yakobo), na Yusufu ( baba wa duniani wa Yesu). Na hii ni mifano michache tuu.

Heshima kwa mifano ya Biblia imenipa ujasiri wa kumwomba Mungu aseme na mimi katika ndoto. Haitokei mara nyingi, lakini ni wazi Bwana amesema nami katika njia hii yenye matunda. 

Siku moja asubuhi na mapema nilipata ndoto ambayo mpaka leo naithamini. Katika ndoto niliona maegesho ya gari niliyoyazoea. Nilipoangalia, rafiki alikuwa anaelekea kwenye gari lililoegeshwa, alifungua mlango wa nyuma, na kumnyanyua mwanae mchanga na kumweka kiti cha nyuma. Yule binti mdogo alikasirika na kuanza kupiga mateke. Kwa subira, taratibu, kwa upole, rafiki yangu alifunga mkanda katika upinzani mkubwa. Hatimaye alimaliza, akaangukia katika kiti cha dereva amechoka sana. 

Nilipokuwa naliangalia tukio, nilishangazwa na kuendelea kwake kwa upole, ambao nilitamani, na vilevile, hasira yake, ambayo ilinifanya nimhurumie. Kama mama mtu mzima, nilijua ukweli--huu ulikuwa ni muda mchache wa uzazi. Zawadi ya uwekezaji wake ungezaa matunda katika maisha ya binti yake, lakini asikate tamaa.

Nilijali sana kwamba hakuweza kujua kitu nilichokuwa nakiona, kwa hiyo katika ndoto nilianza kuita rafiki zangu, "Usikate tamaa! Endelea!" 

Nilipoangalia, rafiki alianza kucheza na simu yake kana kwamba amesikia jambo halisi lakini hakuwa na uhakika chanzo chake. Hakujua nani alikuwa anaongea au kitu gani kinaongelewa. Aliondoa gari lake pasipokuwa na mtizamo wa hekima.  

Baada ya kuamka, niliandika ndoto hiyo na maana yake. Na asubuhi yote niliendelea katika hali ya kuomba na kutafakari maana yake imaweza kuwa ni ipi. 

Masaa machache baadaye, Bwana akaniambia tafsiri yake--nilishtuka. Yule rafiki yangu aliniwakilishamimi katika ndoto, na Yeye ilikuwa ni ile sauti ya kutia moyo. Ndoto ilinijia wakati ambapo nilikuwa nahangaika katika malezi. Alitaka kunijulisha kwamba anajali sana, na kwamba ni wazi familia yangu itavuka majira mengine ya maisha. Ufahamu niliopata ni somo ambalo sijawahi kulisahau kwa sababu kwa namna fulani, naliishi kupitia ndoto. 

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Conversations With God

Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!

More

Tunapenda kumshukuru Susan Ekhoff kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.amazon.com/Prayer-That-Must-Power-Conversational/dp/1496185560/ref=sr_1_1?ie=UTF8&qid=1498693709&sr=8-1&keywords=prayer+that+must+the+power+of+conversational+prayer