Mazungumzo na MunguMfano
Moja ya kumbukumbu zangu nzuri za utotoni zinahusu kabati katika jiko la shambani kwa bibi yangu Easley. Alipoamua kupaka rangi nyekundu jiko lake alifananisha rangi hiyo na kabati. Nilimtembelea mara nyingi nikikaa kwenye kiti nikiwa nimekunja miguu, nikinesa na kuchunguza, nikinesa na kusikiliza, nikinesa na kutafakari utamaduni wa jiko hilo kwa furaha.
Naweza kumwona bibi, akiwa amekaa kwenye chumba kikubwa wakati mvuke ukitokea chini ya mbao zilizowekwa juu ya jiko, na kuku akiokwa juu ya jiko la umeme mezani, wakati wote akiongea. Kuwa na watu kulimtia nguvu bibi. Alinipenda, na nilijua hivyo, nami nilimpenda kwa moyo wangu wote.
Bibi Easley amekuwa mbinguni kwa miaka mingi, lakini mazungumzo tuliyokuwa nayo katika nyumba ile bado yanaishi na kuniinua. Ni sehemu ya urithi wangu.
Miaka mingi iliyopita mama yangu alinizawadia lile kabati jekundu la bibi-- sawa, nilimuomba na hakukataa! Kabati hilo ni kiini cha nyumba yangu, sehemu nzuri ya kusomea vitabu kwa sauti, kukutania na familia na marafiki, na kunesa na mjukuu. Napokuwa sijakaa hapo, moyo wangu umetegwa hapo-- nikitarajia.
Vivyo hivyo kuchukua nafasi yangu katika kabati jekundu kulinileta katika uhusiano wa furaha na bibi yangu, na kukaa karibu nalo nyumbani kwangu napenda sana leo, kufungua Biblia kunatuleta katika kiti ninachokipenda sana kutembea na Bwana kwa muda. Tunapokuwa hatujakaa naye, moyo wake ulio mkubwa unatuonea shauku -kwa kutarajia.
Yesu anapenda kutuvuta katika neno lake tunapoanza kuona kiwango cha upendo wake kwetu na jinsi nasi tunavyoweza kumpenda pia. Tunapokaa naye, hekima ya ufunuo katika maandiko-- mawazo yake na kusudi lake halisi -- vinafunuliwa. Wale ambao kwa uwazi na kwa moyo wote wanayaingia maandiko hawawezi kubaki kama walivyo-- mtazamo wao wa dunia siku zote unafungwa katika maisha yake. Yesu huchukua maneno yake kwenye maandiko na kuyaandika kuwa urithi uishio katika mioyo ya wanadamu. Na anapofanya hivyo, tunabadilishwa kutoka utukufu hadi utukufu.
Kuhusu Mpango huu
Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!
More