Mazungumzo na MunguMfano
Wale wanatamani mazungumzo mazuri na ya ndani na Baba lazima wajifunze kusubiri-- kuamini hekima yake, ukuu wake, mapenzi yake, na majira yake. Lakini kwa nini Mungu wakati mwingine anahitaji kusubiri? Chini kuna njia ya uhakika kuelekea kukomaa, maisha halisi ya maombi tuyatakayo, lakini wakati mwingine tunakosa subira kungoja.
Kama ningeweza, ningetangaza hii kanuni ya kwanza kwa shamrashamra na zulia jekundu: ni vizuri kusubiri upande wa mbele wa maombi, maongezi na Mungu kabla ya kuleta shida zetu. Katika hatua hii ya kufahamu tunakaa na Bwana kugundua nini kiko moyoni mwake. Kusubiri kunaonesha kujikabidhi na kutii mapenzi yake. Tunahitaji hekima yake ili kuomba vyema.
Wakati wanafunzi walipomuomba Yesu awafundishe namnaa ya kuomba, aliwafundisha kusema " Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko Mbinguni" (Mat. 6:10). Tunaweza pia kuanzisha ombi kwa kumuomba tufundishe kuomba. Anapofunua mapenzi yake duniani kama yalivyo Mbinguni, tunakuwa katika nafasi nzuri kufanya maombi kile anachopenda kutupa. Kuomba kwa njia hii kwa pamoja hutimiza shauku ya mioyo yetu. Zoezi hili moja limeimarisha maisha yangu ya maombi. Ninapendekeza furaha za kuomba mapenzi ya Mungu kurudi kwake mwenyewe. Katika uhusiano huu wa mtangulizi, tunangoja kurudi tena kwa Bwana kama Mshauri wa Ajabu.
Wakati mwingine hitaji la kusubiri linakuja baadaye ombi. Aina hii ya kusubiri inahusiana na majira. Si kila wakati ni wa kupokea. “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.” (Mhu 3:1). Wakati halisi utafika, lakini mpaka majira yatimie. Majira halisi yamebarikiwa na majibu ya maombi yetu na mazuri sana.
Hatimaye, kusubiri katika maombi huzaa uvumilivu na uvumilivu ni bure. Wale wanaotamani kukua na kukamilika lazima wafuate ngazi na mteremko vinavyozaa uvumilivu. Biblia inakwenda mpaka sasa kusema kwamba hatua hii ya kuumiza inatakiwa kufurahiwa! Tunaweza kudharau maumivu ya uvumilivu kwa muda huu, lakini baadaye hatutaweza kuondoa faida tuliyoipata. Mungu hatubariki siku zote kwa kutupa mbadala wa hatua ya kuchukua ili kukwepa hatua ya kuvumilia.
Kuhusu Mpango huu
Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!
More