Mazungumzo na MunguMfano
Wakati mwingine hatua sahihi kwenye maombi ni kuachilia. Haya madhabahu ya nafsi ni muda na sehemu maalum tunapoachilia na kukabidhi mapenzi yetu kwa Mungu na kumwachia yeye matokeo yote. Nyakati hizi tunaacha sehemu zetu tunazozipenda jinsi tulivyo mbele zake na kurudi nyuma-- pasipo kujua kitakachotokea baadaye. Huu muda wa kujitenga, unaweza kuonekana kama muda wa hatari sana.
Kuachilia ni msingi wa maombi katika mahusiano na Yesu. Kwa sababu anajua kuachilia mapenzi yetu wenyewe na kwa wale tunaowapenda kunaweza kuwa na maumivu--anajua hili kutokana na uzoefu wake-- Yesu hututegemeza katikati ya hayo yote. Kitendo cha kuachilia, Roho hurejeza nguvu ya neema, uwepo wake unakuwa baraka. Msifu yeye! Tunapoachilia, tunaangukia kwenye mikono ya Upendo.
Hebu tulia na mimi na kumbuka mashujaa wa kwenye Biblia, kwenye historia, na waliopo sasa ambao wameleta mabadiliko kwenye maisha yetu, na walichagua kujikabidhi-- hata kama inamaanisha sadaka au mateso. Pasipo shaka, maumivu ya kujikabidhi ni wakati wao bora, na matukio yanayofuata yanaleta kumbukumbu ya kudumu. Kwa njia hiyo hiyo, tunaposalimisha mapenzi yetu na kufuata mapenzi na wito wa Mungu, tunajiunga na hadithi kuu, safari ya kifalme inayotupeleka mbali zaidi yetu.
Lakini kunatokea nini tunapoona thamani ya maombi ya kuachilia kwetu, lakini tunaogopa sana kuyaomba--bado? Ombi bora linalofuata ni " Bwana, niko tayari kufanywa tayari." Huku kufunguka, kunaachilia nguvu zake kuwezesha kukamilika. "[ Si kwa nguvu zako] kwa maana ni Mungu ambaye mara zote anawezesha ndani yako[akikutia nguvu na kuweka ndani yako nguvu na shauku], ya kupenda na kutenda kwa mapenzi yake na utoshelevu na furaha" ( Wafilipi 2:13). Tunaweza kumwamini Mungu katika kila hatua ya kuachilia. Hakuna jambo gumu kwake, na kila tunachokipenda ni salama Kwake.
Kuhusu Mpango huu
Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!
More