Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mazungumzo na MunguMfano

Conversations With God

SIKU 10 YA 14

Japokuwa alikwenda mbinguni miaka mingi kabla sijaoa na kuwa kwenye familia, nilisikia hadithi nyingi kuhusu bibi ya mume wangu Emma Bald Ekhoff. Kumbukumbu yake ilikuwa juhudi yake katika maombi. Rafiki mmoja alikiri, " maombi ya Emma yaligusa mbingu." Kwa hiyo unaweza kufikiria furaha yangu jioni moja wakati napitia masanduku ya zamani, nilikutana na baadhi ya utani wa Emma wa jikoni-- katika vitu hivyo vilivyopata kutu kulikuwa na jarida! Nilipofungua kajarida kadogo ka kahawia, nilianza kusoma kwa upana. Kalikuwa kameandikwa karibu kila kitu kilichofanyika mwaka 1942. Nilisoma mpaka neno la mwisho, kisha nikafunga na kutunza. Haya ni maombolezo ya kweli: Hakukuwa na chochote mle. 

Machi 3: “Nilinyoosha nguo na soksi mbaya” 

Machi 8: “Wote tulienda kanisani. Douglas alikuwepo kwa chakula cha jioni. Kulikuwa na upepo.” 

Machi 9: “Nilisafisha pishi. Siku nzuri. Niliandika barua.” 

Inafurahisha? Ndiyo, kwa sababu hii ilikuwa na kumbukumbu ya maisha ya familia ya karne ya kati. Lakini ilikuwa ni mwanga kidogo tuu ya mwanga mkubwa. Sentensi ya shauku kubwa katika mwaka huo ilikuwa, " Leo ni siku ya kuzaliwa Dick ( mumewe). Nampenda sana."

Hebu nifikirie mimi. Unadhani ingemaanisha nini kwangu kuwa na mstari wake wa maisha, au lengo lake la mwaka? Unadhani ushauri wa kimungu ungekuwa na ushawishi kiasi gani, au zaidi alipenda nini kuhusu Yesu na kwa nini? Ingekuwa na ukubwa gani kuwa na mstari mmoja uliondikwa wa maombi-- hivyo moja

Kitabu kidogo cha Emma kiko mbele yangu sasa, na ninashangaa: Angeandika tofauti kama angejua ni kiasi gani nilitaka kujua uhusiano wake na Mungu? Angependa uzoefu wake katika maombi kuongezewa kwenye kitabu changu cha maombi? Ni wazi kabisa angependa. 

Miaka sabini kuanzia sasa wakati sanduku letu vitu vyetu dhaifu litakapofunguliwa na kizazi ambacho hatujawahi kukutana nacho, ni salamu gani zitatoka katika mwanga wa dirisha la dari? Je, kuna lolote tunapenda kuzungumza juu ya familia? Kuhusu IMANI? Je, kuna maombi yoyote mioyoni mwetu kwa watakaokuja baada yetu?

Mazunguzo yetu na Mungu ni ya thamani sana-- ya thamani mno, na yana uwezo wa kugusa vizazi ambavyo hatutakutana navyo. 

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Conversations With God

Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!

More

Tunapenda kumshukuru Susan Ekhoff kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.amazon.com/Prayer-That-Must-Power-Conversational/dp/1496185560/ref=sr_1_1?ie=UTF8&qid=1498693709&sr=8-1&keywords=prayer+that+must+the+power+of+conversational+prayer