Mazungumzo na MunguMfano
Kama mama wa shule ya nyumbani, ninatumia sehemu ya majira ya kiangazi kuweka malengo na kupanga mitaala. Kiangazi cha 1999 hakikuwa tofauti, isipokuwa nilikuwa makini sana kwa sababu tulikuwa tunatarajia mtoto wetu wa saba mwezi Oktoba. Ilibidi nifanye kwa umakini kila kitu kabla ya kukosa muda wa kufikiria tena.
Baada ya kupanga kwingi, uamuzi mmoja mzito ulibaki. Samweli, ambaye alikuwa anafikisha miaka minne, alikuwa anashida ya kuongea. Nilihisi mazoezi ya kuongea yangesaidia. Lakini katika ratiba ya shule ambapo kitu laini kama kupokea simu kungemharibu zaidi, na mpango wa kumwona daktari mchana ungeharibu kabisa utaratibu wa familia. Kwa upande mwingine, ingekuwaje kama mwaka huu ungekuwa ni dirisha bora kwa Samweli kupata lugha, na mimi nimekuwa mvivu kumpeleka kwenye darasa rahisi?
Ninakumbuka waziwazi jumamosi mchana nilipotoka kwenda kwenye kutembea na kuongea na Bwana. Nilimweleza kama hivi: "Ninataka kujua hili: Samweli apate mafunzo ya kuongea mwaka huu, au nisubiri afikishe miaka mitano?" Ilikuwa rahisi hivyo na kumaanisha. Bwana hakika angenionesha. Nilijua kwa sababu siku zote alifanya. Kwa hiyo nitatulia kwa kutarajia.
Siku iliyofuatia ilikuwa jumapili, na familia yetu ilikuwa kanisani kama kawaida. Muda wa mahubiri ulipofika, mchungaji wetu Jessica Moffatt alitushangaza kwa kutembea kanisani akiwa amevaa mavazi kamili ya Suzanna Wesley (mama yake John Wesley, mwanzilishi wa dhehebu la Methodist). Katika maneno yaliyofuata, alielezea katika lafudhi ya kiingereza cha zamani jinsi ilivyokuwa kwa mama wa watoto kumi na tisa! Alielezea kumtegemea kwake Mungu katika matukio mengi, na ndipo akarudi kwenye huruma kwa mwanaweSamweli. Nilikaa sawa. “Susanna” aliendelea kuelezea kwamba Samweli Wesley alikuwa na umri wa miakamitano na hakuwahi kuongea hata neno moja. Ghafla siku moja alianza kuongea sentensi kamili.
Nikisiliza kutoka kwangu benchi la tatu mkono wa kushoto, nilikuwa natambua sauti ya Bwana. " Samweli hahitaji kuzungumza mpaka akiwa na miaka mitano. Subiri mpaka mwakani kwa ajili ya mazoezi ya kuongea." Ni amani ilioje, ni ujasiri kiasi gani ulifatia mipango yangu ya kiangazi. Samweli alifanya mazoezi ya kuongea mwaka uliofuatia, na kuongea kwake kulibadirika haraka sana.
Bwana anatutaka tumwulize maswali maalum na tuongozwe na mapenzi yake. Kwa uhakika anajali sana ufasaha wetu.
Kuhusu Mpango huu
Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!
More