Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mazungumzo na MunguMfano

Conversations With God

SIKU 3 YA 14

Bwana hutuchunga kwa sauti yake nasi tunamwitikia kwa sauti zetu. Je si mantiki Yeye anayejiita Neno siku zote anawasiliana? na kwamba Yeye, aliyetuumba kushirikiana naye, alijitoa ili tumrejee, anajua tuyawazayo kabla hatujatamka,anapenda kusikia sauti zetu tukiongea naye? 

Kwa shukrani, mazungumzo haya bora zaidi hayategemei uzuri wetu, mafanikio yetu, au ubora wa maswali yetu. Upendeleo wa kusikilizwa na kusikiwa msingi wake ni dhabihu ya Yesu pekee.

Maongezi yanaanza Bwana anapotutafuta. Mungu ni pendo na upendo wake lazima ufike kwa mahusiano. Wajibu wetu ni kutambua sauti yake na kumwitikia. Naye kwa uaminifu anatujibu. Katika mazungumzo tunafurahia uwepo wake, tunatii na kuamini. Nadhani mazungumzo ya namna hii ndiyo Paulo aliyasisitiza aliposema " ombeni bila kukoma." Aidha tunamsikiliza Bwana au tunaeleza kitu kwake na tukisubiri kwa matarajio majibu yake. Hii ni kazi na furaha ya maisha yetu. Hatimaye, tunakuta hatuwezi kuishi bila Bwana wa maongezi. Hatuna budikuomba.

Maombi pasi na shaka hujenga na huimarisha. Maongezi yetu na Mungu huleta hekima na amani. Tunapokuwa hatujui namna ya kuendelea, maombi ni hatua sahihi. Ni kufunguliwa. Ni rahisi. Ni pumziko. 

Kuongea na kumsikiliza Mungu na muitikio wa mahitaji yetu ya mawasiliano Naye-- sasa hivi. Kama mazungumzo sahihi ya Tevya na Mungu katika Fiddler on the Roof, tunaongea na kusikiliza kwa siku zetu za kawaida. Bwana siku zote anaita na kusubiri kwa ajili ya usikivu wetu. Nimekuwa siku zote nashangaa kwa nini inatufhukua muda mrefu kutegemea mahusiano yetu. Tunapogeuka, tunajikuta katikati Yake--Jibu.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Conversations With God

Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!

More

Tunapenda kumshukuru Susan Ekhoff kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.amazon.com/Prayer-That-Must-Power-Conversational/dp/1496185560/ref=sr_1_1?ie=UTF8&qid=1498693709&sr=8-1&keywords=prayer+that+must+the+power+of+conversational+prayer