Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mazungumzo na MunguMfano

Conversations With God

SIKU 5 YA 14

Nyuma miaka ya tisini, Richard ( mume wangu) na mimi tulianza kujadili uwezekano wa kubadilisha ushirika wa kanisa la miaka karibu kumi. Tulikuwa tunatamani zaidi aina ya kuabudu kwa kisasa na hatukuona dalili zozote za kubadirika. Baada ya miezi mingi, tukapunguza chaguo letu mpaka makanisa mawili au matatu na tulikuwa tunatarajia kuondoka. 

Wakati huo, tulikubaliana kuhudhuria wikendi ya kufanywa upya kiroho. Wanaume walihudhuria kwanza, na wanawake wakafuata wiki mbili zilizofuata. Tulifurahi sana kuhusu nafasi ya kuwa na Bwana mbali katika kipindi hiki cha " katikati ya makanisa".

Masaa sabini na mbili ya Richard yakawa uamsho binafsi-- niliweza kuona usoni kwake alipoingia mlangoni jumapili jioni. Aliponisimulia, nilianza kutamani zamu yangu ifike kuhudhuria. 

Baada ya kuniambia mambo mengi, mwishowe alifika kwenye somo ambalo kiutaalam aliliacha mpaka mwisho. Akizungumza kwa uhuru, alielezea kwamba wakati wa kongamano Bwana alimfunulia kwamba tusihame kanisa-- tubaki tulipo. Nilipokuwa natafakari maneno ya kumjibu, niliropoka kwamba Bwana hajanifulia ukweli huomimi na yawezekana alikosea, ambapo kwa hekima alijibu basi tusubiri tuone.

Karibu nusu ya siku zangu za kongamano langu, Bwana alizungumza nami pia. Kwa muda nilikuwa sijielewi, na baadaye nikaelewa kwa uhakika: tunatakiwa kubaki kwenye kanisa la nyumbani. Basi. Makusudi yangu ya awali yaligonga mwamba wa Mungu, mapenzi yasiyotikisika kama gari lenye mwendo kasi likigonga uzio wa chuma.

Nikitetemeka na kuugua, nilianza kulia kwa huzuni. Utii wangu ulihitajika. Tulitakiwa kubaki, lakini muda huo sikuweza kuelewa mawazo ya Mungu. Ilichukua uelewa wa miaka mingi kuelewa kwa nini. Wakati huo tuliamua kutii na tukabaki.

Kilichofuata ilikuwa na kidonda kwenye tabia yangu ya ubishi, ikifuatiwa na somo la unyenyekevu. Baadhi ya masomo nayoyathamini niliyapata kwa sababu nilitii na nililazimika kujifunza.

Kwa mshangao wangu kanisa letu nalo likapitia kufanywa upya kwa wakati wa Mungu. Sasa najua kutokana na uzoefu kwamba Bwana anaweza kumbadili yeyote-- hata mimi. Na kuona uamsho katika kanisa la nyumbani ilistahili kusubiri. Baraka siku zote zinafuata utii.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Conversations With God

Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!

More

Tunapenda kumshukuru Susan Ekhoff kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.amazon.com/Prayer-That-Must-Power-Conversational/dp/1496185560/ref=sr_1_1?ie=UTF8&qid=1498693709&sr=8-1&keywords=prayer+that+must+the+power+of+conversational+prayer