Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Bwana Yesu atakasa hekalu. Kwa tendo hili, twaona kwa sehemu kazi yake ya kutakasa mioyo ambayo ni hekalu la Roho Mtakatifu. Akemea uovu, na kutangaza utakatifu unaotarajiwa kwa walio wake. Awapa vipofu nuru ili kuonyesha awezavyo kufumbua macho ya rohoni, watu wamfahamu yeye na mapenzi yake. Awatia nguvu wasiojiweza kwa jinsi ileile atutiavyo uweza wa kumtumikia. Na kama hatumzalii matunda atangaza hukumu.Mwisho, afundisha wanafunzi uweza atakaowavika wote watakaomwamini:Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka(m.21). Linganisha neno hili na lingine la Yesu linalopatikana katika Yn 14:12:Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Maana yake, yote tunayofanya sisi, yategemea kwamba Yesu yuko kwenye kiti cha enzi mbinguni kama Bwana wa Kanisa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz