Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Hakuna tukio lolote litakaloweza kumwangamiza aaminiye. Inawezekana litazaa huzuni moyoni mwake, lakini Mungu atamsimamia. Anazungukwa na malaika, na ahadi za Mungu zinampa tumaini katika taabu. Na zaidi ya hayo, hayupo peke yake taabuni. Bwana mwenyewe yupo pamoja naye. Je, unajua huyu Bwana ni nani? Ni Mungu pamoja nasi, ni Imanueli, ni Yesu Kristo. Ndivyo malaika alivyomwambia Yusufu, huyu alipogundua kwamba mchumba wake, Mariamu, alikuwa na mimba:Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi(Mt 1:23). Ukiwa pamoja na Yesu, hakuna jambo linaloweza kukuangamiza. Na mwisho wa taabu yako ni nini? Uzima wa milele na wokovu wa milele, kwa sababu katika m.16 Mungu anaahidi:Nitamwonyesha wokovu wangu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz