Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

SIKU 1 YA 31

Hii ni habari ya Bwana Yesu kuingia Yerusalemu akiwa tayari kuuawa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. Lakini badala ya kuingia kwa simanzi na majonzi, anaingia kwa mvumo wa kishindo cha mfalme. Kupanda punda kunaashiria unyofu wa moyo na kuleta amani. Hivyo Yesu anatangaza kuwa ni Mfalme mpole, mnyenyekevu asiyejivunia ukuu wake. Anatawala kwa upole wote wamwaminio. Zingatia kuwa Yesu anawatangazia wote wanaokubali kuwa raia wake, kwamba wawe wapole na wanyenyekevu kama mfalme wao:Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi(Mt 5:5).

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz