Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Viongozi wa dini nyakati za Yesu walijitukuza na kupenda waheshimiwe. Walifundisha torati, lakini waliongeza sheria zao, tena zisizotekelezeka. Yesu alionya watu watii mafundisho ya kweli, na wajihadhari na mienendo yao. Utumishi umpendezao Mungu ni ule wa kujishusha na kunyenyekea kwake. Vipi na kujitukuza kwa wahudumu wa Injili siku hizi, kupo au hakupo? Mimi na wewe tunahudumu Injili kwa unyenyekevu? Onyo hili la Bwana Yesu lafaa sana kuzingatiwa na wote wanaoeneza Injili nyakati zetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz