Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Neno la leo ni mwendelezo wa mafundisho ya hali itakavyokuwa siku za mwisho. Hata maeneo ya ibada yatashambuliwa au kuchafuliwa. Dhiki na mateso ya kutisha yatashamiri, na uzushi wa kuwepo kwa Kristo mahali pa siri utasikika. Manabii na makristo wa uongo watainuka na kupotosha wengi. Lakini, Mungu ashukuriwe! Ameikatisha dhiki ili wateule wake waokoke. Yesu ameyabainisha haya kwa sababu ya upendo ili tusiwe gizani. Tafakari matukio yote. Kuyaelewa kutakusukuma ukeshe ukimngoja Bwana atakaporudi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz