Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

SIKU 5 YA 31

Mungu ndiye Mfalme aliyealika na anayeendelea kualika watu waingie katika furaha ya ufalme wake. Anatumia watumishi mbalimbali kualika. Wengi wanaukataa mwaliko, na Mungu atawaacha katika upotevu wao. Lakini hakati tamaa bali anaendelea kualika wengine, wema kwa wabaya. Hata hivyo ni muhimu kutambua kuwa yeyote anayeamua kuingia hiyo furaha ni lazima akubali kuvikwa vazi la wokovu, ambalo ni imani katika Kristo. Twaitwa tujikabidhi kwa Yesu ili atutakase na kutuvika vazi la arusi. Nabii Isaya alisema,Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu(Isa 61:10). Je, hii pia ni furaha yako?

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz