Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Huu ni mfano wa Mungu alivyojichagulia Israeli wawe watu wake. Lakini hawakuwa waaminifu kwake. Ndipo akawaletea manabii wawaonye. Hawakuwakubali. Hatimaye Mungu aliwapelekea Mwanawe Yesu, ila wakamwona kikwazo kwao, wakamwua. Je, sasa Mungu anataka nini? Anataka mimi na wewe tuwe watu wa upande wake hapa duniani. Ni kwa namna gani tutafanyika watu wa upande wa Mungu? Kwa kumwamini Yesu Kristo. Leo, mimi na wewe tunaitwa tumwamini Yesu ili tufanyike taifa jipya la Mungu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz