Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

SIKU 3 YA 31

Wakuu wa dini waliudhiwa na Yesu alivyopindua meza zao hekaluni. [Yesu]akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa(21:12). Kwa tendo hili Yesu aliwapa fundisho na nafasi ya kutambua dhambi zao. Waone jinsi wasivyotumika ipasavyo nyumbani mwa Mungu. Hata hivyo hawa watumishi katika hekalu la Mungu hawakuona haja ya kutubu. Matokeo yake ni nini? Yesu anawapa watoza ushuru na makahaba wamwaminio kutangulia mbele ya makuhani kuingia katika ufalme wa mbingu! Hili ni onyo vilevile kwaWakristo waishio katika mazoea ya kidini tu bila kutubu kweli.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz